KIKWETE AELEZA RAIS SAMIA ALIVYOPELEKA FURAHA NA NEEMA KWA WATUMISHI WA UMMA

Kwenda kupandisha madaraja Watumishi 219,042, ongezeko la mishahara kwa 35.1%, ongezeko la kima cha chini sekta binafsi.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imefanya maamuzi mbalimbali makubwa katika kuhakikisha maslahi ya Watumishi wa umma nchini yanaboreka hivyo kuwakumbusha Maafisa tawala na Rasilimali watu kutekeleza wajibu wao na kuleta furaha kwa watumishi wa umma ili kwa upande mwengine nao wapeleke furaha na neema kwa Watanzania.

Kikwete ameyasema hayo Jana akiwa mgeni rasmi kwenye mkutano wa Maafisa tawala na Rasilimali watu uliofanyika katika uliofanyika Ukumbi wa AICC, Jijini Arusha. 

"Uamuzi wa hivi karibuni wa Serikali kupandisha madaraja watumishi 219,042 ni hatua ya kihistoria katika kuimarisha utumishi wa umma nchini Tanzania baada ya hatua hii kupata ridhaa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na ongezeko la mishahara ya watumishi wa umma (2025): +35.1%, ongezeko la kima cha chini sekta binafsi 2025/26 kwa 33.4% ambapo sekta mbalimbali zinakwenda kunufaika na maboresho haya ikiwemo afya, elimu, kilimo, mawasiliano, usafirishaji, nishati, viwanda, biashara, hoteli, michezo, uvuvi, baharini, madini, utamaduni n.k." Alisema Kikwete akiongea kwenye mkutano huo.

Matokeo haya kitakwimu yanaonyesha kasi ya mageuzi ya kiutumishi chini ya Serikali ya Rais Samia ambayo inaonyesha uongozi wa kimkakati unaoweka mbele ustawi wa watumishi na ufanisi wa taasisi za umma.


 

Post a Comment

0 Comments