Na Ally Mandai
Uongozi wa Klabu ya Young Africans Sports Club umetangaza kumfuta kazi Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Pedro Gonçalves.
BOFYA HAPA SIKILIZA GOSPEL SINGELI YA PATRICK NAUBUTU -MBINGUNI (OFFICIAL AUDIO)
Taarifa ya Yanga iliyotolewa jioni hii imesema Uongozi wa Klabu unamshukuru Kocha Pedro Gonçalves kwa mchango wake alioutoa ndani ya klabu yetu na unamtakia kila la kheri katika majukumu yake yajayo.
Katika kipindi hiki kikosi cha Yanga kitakuwa chini ya uongozi wa Kocha Abdihamid Moalin pamoja na Kocha Patrick Mabedi hadi mwisho wa msimu.


0 Comments