VIONGOZI WA DINI WAHIMIZWA KUSIMAMIA AMANI NA UTULIVU

Na.Mwandishi Wetu.

Viongozi wa Dini wamehimizwa kusimamia Amani katika maeneo yao kwani ndio msingi Mkubwa wa Maendeleo katika Nchi.

Rai hiyo imetolewa leo April 24,2026na  Mkuu wa Wilaya ya Longido Mkoani Arusha, Salum kalli, katika kikao cha Kamati ya Haki na Amani Wilayani humo.

"Nchi yeyote ili ipate Maendeleo inategemea sana Amani na Utulivu kwa Watu wake,ndio Maana Ninyi mmepata fursa katika Madhehebu yenu,Kuhubiri Amani,Upendo na Utulivu kwamba sisi Wanadamu tumepata nafasi ya Kutambua Mema na Mabaya.

Na niendelee kutoa Shukrani Nyingi,Kwenu Viongozi kwa kuwa kila Ziara,tunayofanya katika Vijiji na kata, Viongozi wa Kiroho,mmekuwa Bega kwa bega na Serikali,kuhakikisha Amani inapatikana pamoja na Ustawi wa Wananchi katika maeneo husika.

Hivyo basi Niwaombe Viongozi wa Kiroho,tuwe sehemu ya kusuluhisha Migogoro ya Kidini,katika maeneo yetu, Ili taasisi zetu ziendelee kufata misingi ya Amani na utulivu,katika Nchi yetu,kwani mna dhamana kubwa sana mliyopewa Kiroho, ili kuhakikisha Amani inapatikana katika jamii zetu zinazotuzunguka,Amesema Kalli;'

Kwa Upande wake, Katibu wa Baraza la Ushauri la Wazee Wilaya, Mch.Benny Lendiy,amewataka Viongozi hao,kujiepusha kuchanganya Dini na Siasa, ili kubaki katika Misingi ya Kiroho na kuendelea kuliombea Taifa.

Aidha Benny,amempongeza Mhe.Kalli kwa kuwatanguliza,na Kuwashirikisha mambo mbali mbali ya Wilaya pale wanapohitajika,na kusema ndani yake wanaona ni Kiongozi Mnyenyekevu,Msikivu na Anaeishi na Shida za Watu.

Kikao hicho cha Kamati ya Haki na Amani Wilaya chini ya Mwenyekiti wake Sheikh Ramadhan  Mpangala, kimefanyika katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya, na kuhudhuriwa na Kamati ya usalama, pamoja na viongozi wa madhehebu mbali mbali.



Post a Comment

0 Comments