UDSM NA HARVARD WAANZA MAZUNGUMZO YA USHIRIKIANO WA AI KUIMARISHA ELIMU NA UTAFITI

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mkuu wa Harvard Kennedy School, Prof. Jeremy M. Weinstein baada ya mazungumzo yao huko Marekani.

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimeingia katika mazungumzo ya ushirikiano wa kimkakati na Chuo Kikuu cha Harvard, Marekani, yakilenga kuimarisha matumizi ya Akili Mnemba (AI) katika elimu, utafiti na uchambuzi wa taarifa.

Mazungumzo hayo yalianzishwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alipokuwa katika ziara ya kikazi nchini Marekani.

Ushirikiano huo unalenga kujenga uwezo wa kutumia AI kwa ufanisi katika kufundishia, kuongeza kasi ya tafiti, na kurahisisha uchakataji wa taarifa nyingi kwa wakati mfupi, eneo ambalo linazidi kuwa muhimu katika vyuo vikuu duniani.

Katika kipindi ambacho taasisi za elimu ya juu zinakabiliana na changamoto na fursa zinazotokana na AI, hatua ya UDSM kuingia katika mazungumzo na Harvard inaonekana kama mkakati wa mapema wa kuhakikisha Tanzania haiwi nyuma katika mapinduzi ya teknolojia.

Akizungumza katika kikao hicho, Dkt. Kikwete alisisitiza umuhimu wa matumizi sahihi na yenye uwajibikaji ya AI, akibainisha kuwa teknolojia hiyo inaweza kuwa nyenzo muhimu ya kuboresha ubora wa elimu na utafiti iwapo itasimamiwa vyema.

Kwa upande wa Harvard, majadiliano yalihusisha viongozi na wataalamu waandamizi, akiwemo Mkuu wa Harvard Kennedy School, Prof. Jeremy M. Weinstein, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Maendeleo ya Kimataifa (CID), Dkt. Fatema Sumar.

Unahangaika na maisha? Huna kazi, biashara haisongi na pesa zimekuwa tatizo? Profesa Bahari Kisiki, mganga gumzo anayepatikana Njia Panda ya Uyole – Mbeya anatajwa kusaidia watu wengi kubadili maisha yao kwa kuwapa suluhisho la changamoto za pesa, kazi, biashara, mahusiano na kusafisha nyota.

USIENDELEE KUTESEKA WAKATI SULUHISHO LIPO. PIGA SIMU SASA +255 792 70 70 70 NA UPATE MSAADA WAKO MAPEMA.


Post a Comment

0 Comments