Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesisitiza umuhimu wa mshikamano wa Kitaifa ikiwa ni namna muhimu ya kuwaenzi waasisi wa Muungano, Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume.
Makamu wa Rais ametoa msisitizo huo, wakati wa Tamasha la Usiku wa Mtanzania ikiwa ni shamrashamra za maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano, lililofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Amesema ni msisitizo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vijana na watanzania kwa ujumla kuhusu kuwa na mshikamano kulinda umoja na amani.
Makamu wa Rais amewasihi watanzania kutafakari na kujielekeza katika kujenga mshikamano ni kuhakikisha Muungano unalindwa.
Amesisitiza umuhimu wa kuvumiliana katika utoaji wa mawazo,kushauriana kujenga utaratibu wa kukubaliana hata katika masuala yanayotoafutiana mawazo.
Awali akitoa neno la utangulizi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema Tamasha hilo hilo linalenga amani, umoja na mshikamano miongoni mwa wananchi wa pande zote mbili za Muungano.
Amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa kufanikisha kutatuliwa hoja 22 kati ya 25 za Muungano. Pia amempongeza Makamu wa Rais, kwa kuongoza Kikao cha Kamati ya Pamoja na kufanikisha kutatuliwa kwa hoja ya uingizaji sukari katika soko la Tanzania Bara hivyo kuufanya Muungano kuwa imara zaidi.
Aidha, amesema shughuli mbalimbali zimefanyika katika Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano, zikiwemo uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo, makongamano na mjidala kuhusu Muungano ikilenga kutoa elimu kwa wananchi.
Aidha Serikali zote mbili kupitia Vyama vya Michezo zimeshirikiana katika kuandaa mashindano ya mpira wa miguu ya Kombe la Muungano yanayoendelea Zanzibar. Ameongeza kwamba, elimu ya Muungano itatolewa pia katika Msafara wa Muungano (Muungano Caravan) ambao utazinduliwa Mei 03, 2026 jijini Dar es Salaam na kuhusisha wilaya zotMakamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
amesisitiza umuhimu wa mshikamano wa Kitaifa ikiwa ni namna muhimu ya
kuwaenzi waasisi wa Muungano, Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage
Nyerere na Hayati Abeid Amani Karume.
Makamu wa Rais ametoa
msisitizo huo, wakati wa Tamasha la Usiku wa Mtanzania ikiwa ni
shamrashamra za maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano, lililofanyika
katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es
Salaam.
Amesema ni msisitizo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa vijana na watanzania kwa
ujumla kuhusu kuwa na mshikamano kulinda umoja na amani.
Makamu wa Rais amewasihi watanzania kutafakari na kujielekeza katika kujenga mshikamano ni kuhakikisha Muungano unalindwa.
Amesisitiza
umuhimu wa kuvumiliana katika utoaji wa mawazo,kushauriana kujenga
utaratibu wa kukubaliana hata katika masuala yanayotoafutiana mawazo.
Awali
akitoa neno la utangulizi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
(Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema
Tamasha hilo hilo linalenga amani, umoja na mshikamano miongoni mwa
wananchi wa pande zote mbili za Muungano.
Amempongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein
Ali Mwinyi kwa kufanikisha kutatuliwa hoja 22 kati ya 25 za Muungano.
Pia amempongeza Makamu wa Rais, kwa kuongoza Kikao cha Kamati ya Pamoja
na kufanikisha kutatuliwa kwa hoja ya uingizaji sukari katika soko la
Tanzania Bara hivyo kuufanya Muungano kuwa imara zaidi.
Aidha,
amesema shughuli mbalimbali zimefanyika katika Maadhimisho ya Miaka 62
ya Muungano, zikiwemo uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo,
makongamano na mjidala kuhusu Muungano ikilenga kutoa elimu kwa
wananchi.
Aidha Serikali zote mbili kupitia Vyama vya Michezo
zimeshirikiana katika kuandaa mashindano ya mpira wa miguu ya Kombe la
Muungano yanayoendelea Zanzibar. Ameongeza kwamba, elimu ya Muungano
itatolewa pia katika Msafara wa Muungano (Muungano Caravan) ambao
utazinduliwa Mei 03, 2026 jijini Dar es Salaam na kuhusisha wilaya zote.




0 Comments