KAPTENI IBRAHIM TRAORE: BURKINAFASO ISAHAU KUHUSU DEMOKRASIA

 Kapteni Ibrahim Traoré, ambaye aliingia Madarakani kwa njia ya Mapinduzi miaka mitatu iliyopita, amesema kuwa Waafrika wengi hawahitaji Utawala wa Kidemokrasia na kwamba Burkina Faso ina mfumo wake wa Serikali, bila kutoa maelezo ya mfumo huo.

Alipoingia Madarakani, Traoré aliahidi kurejesha Utawala wa kidemokrasia ifikapo Julai 7, 2024, lakini miezi miwili kabla ya tarehe hiyo, utawala wake wa kijeshi uliongezwa kwa miaka mingine mitano.

Mnamo Januari, Serikali ya Ouagadougou ilitangaza kuwa inapiga marufuku vyama vyote vya kisiasa kwa nia ya kuijenga upya nchi.

Katika mahojiano Traoré alisema: “Watu wanapaswa kusahau kuhusu Demokrasia. Demokrasia si yetu.”

Alitoa mfano kwa nchi ya Libya ambayo ilitawaliwa kwa takribani miaka 40 na Kanali Muammar Gaddafi, ambaye alitawala kama Dikteta lakini utawala wake uliwapatia Walibya makazi, elimu na huduma za afya bure.

Aliuawa katika uasi ulioungwa mkono na nchi za Magharibi. Baadae nchi iligawanywa katika serikali mbili zinazopingana na kuibuka vikundi vingi vyenye silaha.


 

Post a Comment

0 Comments