DC MWEMA AKABIDHIWA RASMI JENGO LA OFISI YA MKUU WA WILAYA KITETO

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto  Mheshimiwa Remidius Mwema  jana tarehe 28 Aprili,2026 amekabidhiwa rasmi jengo la ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kiteto lenye thamani ya Shilingi bilioni 1.7 lililopo Mtaa wa Msakasaka, Kata ya Bwagamoyo, Tarafa ya Kibaya Wilayani Kiteto.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mheshimiwa Queen Sendiga amekabidhi jengo hilo baada ya kukagua na kujiridhisha na hatua ya ukamilishaji wa Mradi huo wenye vyumba 35 na ukumbi wa Mikutano ambao umetekelezwa kwa mfumo wa force akaunti tangu  kuanza kwake  tarehe 30 Machi,2023.

“Nawapongeza wataalamu na mafundi wote walioshiriki kufanikisha ujenzi huu,uzuri wa jengo hili ni lazima uende sambamba  na utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kutoa tafsiri halisi ya uwajibikaji na utendaji kazi na huduma kwa wananchi” Mhe. Sendiga.

Aidha, Mhe. Mwema ameishukuru Serikali kwa kufanikisha mradi huo mkubwa na kuahidi kutekeleza kikamilifu maelekezo yote ya Mkuu wa Mkoa kuhusu Mradi pamoja na kuendelea kuifanya ofisi hiyo kuwa kimbilio la kila mwananchi wilayani kiteto “ Ni kweli jengo  linapendeza sana  kwa muonekano wake, ahadi yetu ni kuongeza furaha mioyoni mwa wananchi kwa usikivu  na huduma kwa makundi yote ya wananchi, bahati nzuri miundombinu ya ofisi hizi inawezesha na watu wote wenye mahitaji maalum kuhudumiwa” Mhe. Mwema

Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Msakasaka kata ya Bwagamoyo  Mwangao Sadick Mpalila amesema mradi huo umesogeza karibu huduma kwa wananchi na kwamba  uwepo wa Jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya katika mtaa huo pia itasaidia wananchi wengi zaidi  sasa kupata huduma kwa haraka na wakati mmoja.


 

Unahangaika na maisha? Huna kazi, biashara haisongi na pesa zimekuwa tatizo? Profesa Bahari Kisiki, mganga gumzo anayepatikana Njia Panda ya Uyole – Mbeya anatajwa kusaidia watu wengi kubadili maisha yao kwa kuwapa suluhisho la changamoto za pesa, kazi, biashara, mahusiano na kusafisha nyota.

USIENDELEE KUTESEKA WAKATI SULUHISHO LIPO. PIGA SIMU SASA +255 792 70 70 70 NA UPATE MSAADA WAKO MAPEMA.

 

Post a Comment

0 Comments