WALIMU MASAMA MAGHARIBI WAPONGEZWA KWA KAZI NZURI

Mkuu wa wilaya ya Hai amewapongeza Walimu waliofanya Vizuri katika Mhula wa masomo Mwaka 2025-2026 na kuwapa Motisha ya vyeti na fedha kwa kufaulisha watahiniwa wa Darasa la Saba, Kidato cha Pili na cha nne

Aidha Mh Bomboko amewataka maafisa elimu ngazi zote na wataalumu kuhakikisha wanaweka mpango mkakati thabiti utakaonyanyua kiwango cha ufaulu kwa madarasa yenye mitihani ya Taifa

Pamoja na Mikakati ya kuongeza Ufaulo DC ameweka mipango ya Serikali wilayani Hai katika Kujenga Madarasa mapya na Matundu ya Vyoo “Mkurugenzi tumepewa maelekezo na Mh Rais kupitia waziri Mkuu Halmashauri zijenge matundu ya vyoo ndani ya Miezi sita, SISI WILAYA YA HAI kazi hii tutaifanya kwa miezi Mitatu tuwe tumekamilisha zoezi la ujenzi wa vyoo kwenye shule zenye uhitaji”






Post a Comment

0 Comments