TAKUKURU KINONDONI YABAINI UTEKELEZAJI WA MIRADI NJE YA MUDA,YAFUATILIA MIRADI YA BIl.5

Na Moshi said 

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU  wilayani kinondoni imesema imeendelea na jitihada za kufuatilia utekelezaji wa matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa umma na kufanya uchunguzi wa tuhuma mbalimbali wilayani humo.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Taasisi hiyo Mkoa wa  kinondoni Christian Nyakizee wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya mafanikio ya Utendaji kazi wa Taasisi hiyo wilayani humo kuanzia mwezi Oktoba hadi Disemba 2025.

Nyakizee amesema katika kuzuia vitendo vya Rushwa TAKUKURU  inalo jukumu la kufuatilia matumizi ya fedha zilizoelekezwa kwenye  miradi ya maendeleo ili kuhakikisha kuwa miradi hiyo inatekelezwa kwa ufanisi lakini pia thamani ya fedha kwenye miradi inaonekana.

"Kama mnavyofahamu Takukuru ni jukumu letu kufuatilia miradi yote ya maendeleo na kuona inatekelezwa  kwa wakati na ufanisi unaostahili katika kuzuia hujuma na matumizi mabaya ya fedha" amesema Nyakizee

Mkuu huyo wa Takukuru wilayani humo amesema katika ufuatiliaji wa miradi  miwili ya maendeleo wilayani humo katika sekta ya miundombinu(Barabara) ambazo ni ujenzi wa Barabara ya Gemma na Barabara ya Nyaishozi zilizopo kata ya Bunju zenye thamani ya Bilioni 5, ambapo katika ufuatiliaji huo ilibaini kuwepo kwa ongezeko la muda wa utekelezaji wa miradi hiyo kutokana na sababu mbili 
Ikiwemo mabadiliko ya hewa kuchewa kwa malipo na ombi la msamaha  wa kodi wakiwemo wakandarasi, washauri na wasimamizi wa miradi hiyo ili kuhakikisha  miradi inakamilika ndani ya muda wa nyongeza waliopatiwa kwa kuzingatia ubora na thamani ya fedha.

Aidha Mkuu huyo wa Takukuru amesema katika wilaya hiyo kuna malalamiko 72 yalipokelewa katika kipindi hicho ambapo malalamiko 25 yalihusu vitendo vya Rushwa na malalamiko 47 hayakuhusu vitendo vya Rushwa malalamiko 25 yalihusu  Rushwa na uchunguzi wake unaendelea na upo katika hatua mbalimbali.

Vilevile Nyakizee amesema  kuanzia mwezi Januari hadi  Machi wameweka mikakati ya utendaji kazi uanohusisha kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na wadau  kuhusu kuzuia Rushwa 
katika miradi ikienda sambamba na kufuatilia utekelezaji wa mapendezo ya program  ya Takukuru rafiki.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Takukuru ametoa rai kwa wananchi wote kujiepusha na vitendo  vya Rushwa na kushikiriki kikamilifu katika kuzuia vitendo hivyo katika maeneo yao.


 

Post a Comment

0 Comments