Na Ally Mandai.
Klabu ya Simba imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 (milioni tano) kwa kosa la kuingia kwenye uwanja wa Amaan, Zanzibar kupitia mlango usio rasmi kuelekea mchezo tajwa hapo juu Machi Mosi, 2026, kinyume na matakwa ya kanuni ya 17:21 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Klabu ya Simba imetozwa faini ya Sh. 5,000,000 (milioni tano) kwa kosa la kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia kwenye uwanja wa Amaan, ambapo walitumia chumba cha kufanyia mikutano ya Wanahabari kwa shughuli hiyo kabla ya kuanza mchezo, kinyume na matakwa ya kanuni ya 17:20 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 17:62 ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.
Klabu za Young Africans na Simba zimetozwa faini ya Sh. 5,000,000 (milioni tano) kila moja kwa kosa la walinzi wake kugombana na kutoleana lugha ya matusi, jambo lililozua taharuki na kuchafua taswira ya mchezo huo wakati klabu ya Simba ikiwasili uwanjani hapo.
Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Klabu.
Klabu ya Simba italazimika kulipa gharama za matengenezo ya mlango wa kuingilia chumba cha kufanyia mikutano ya Wanahabari ambao walinzi wake waliuvunja ili kulazimisha timu hiyo kuingia na kutumia chumba hicho kwa ajili ya kuvalia kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
TANGAZA NASI SASA,UWAFIKIE MAMILIONI YA WATEJA:Piga 0654414804.

0 Comments