SIMBA YAICHAPA B19,KUKUTANA NA DODOMA JIJI 16 BORA
Na Ally Mandai
Klabu ya
Simba imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la CRDB
baada ya kuibuka na ushindi mnono wa 2-0 dhidi ya B19 FC.
Mabao ya Simba yalipatikana kupitia kwa Inno Loemba dakika ya 22 na Clatous Chama dakika ya 77.
Mchezo huo wa hatua ya 32 bora ulipigwa katika dimba la Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni jijini Dar es Salaam.
B19
FC, ambayo inashiriki ligi ya Championship, ilijaribu kuonyesha
upinzani lakini ilishindwa kuhimili kishindo cha Wekundu wa Msimbazi.
Baada ya ushindi huu, Simba sasa itakutana na mshindi kati ya Dodoma Jiji FC katika hatua ya 16 bora.
Mechi zilizopigwa leo Jumamosi, Machi 7, 2026, katika hatua ya 32 Bora ya Kombe la CRDB.
Namungo FC 4 – 1 Kagera Sugar
Geita Gold FC 4 – 1 Nyika FC
Pamba Jiji 2 – 1 Transit Camp
Mashujaa FC 0 – 0 KenGold FC (Mashujaa imeshinda kwa penalti 5-3).
0 Comments