Serikali
inaendelea kuthamini mchango wa sekta binafsi katika kukuza Uongozi
bora, Ajira stahiki pamoja na kuimarisha usawa wa kijinsia mahali pa
kazi.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu –
Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo, wakati akifungua Kongamano
la Women’s Leadership Forum Machi 28, 2026 jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Kisuo amesema mafanikio ya taifa yanategemea ushirikiano madhubuti kati
ya Serikali na waajiri katika kujenga mazingira ya kazi yaliyo salama,
jumuishi na yanayoheshimu haki za wafanyakazi wote bila ubaguzi.
Aidha,
amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuongoza juhudi za kuweka sera na mikakati
inayowawezesha wanawake na vijana kushiriki kikamilifu katika uchumi wa
taifa.
0 Comments