Na Ally Mandai.
Shirikisho la Soka barani Afrika, CAF, limechukua uamuzi mzito na wenye uzito mkubwa katika historia ya mashindano yake baada ya kubadili rasmi matokeo ya mchezo wa fainali.
Kwa mujibu wa taarifa zinazosambaa kupitia mitandao ya kijamii, bodi ya CAF imeamua kuwa Senegal wamepoteza mchezo huo kwa “forfeit”, hatua inayomaanisha wamekosa sifa za kuendelea kushikilia ushindi wao wa uwanjani.
Kutokana na uamuzi huo, Morocco wametangazwa mabingwa kwa ushindi wa mabao 3–0 kwa mujibu wa kanuni na taratibu za mashindano.
Maamuzi hayo yamefuta kabisa matokeo ya awali ya uwanjani yaliyokuwa yakionesha ushindi wa 1–0 kwa upande wa Senegal, na badala yake kuipa Morocco ushindi wa mezani.
Hatua hii imeibua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa soka, wachambuzi na mashabiki, wengi wakijiuliza juu ya misingi ya uamuzi huo na athari zake kwa haki na uadilifu wa mchezo.
CAF wanasema kuwa Senegal wamevunja kifungu namba 84,huku kanuni za AFCON zikisema timu ikigoma au kutoka uwanjani watakuwa wamepoteza mchezo husika.



0 Comments