MWAMUZI HAMDANI SAID AMEFUNGIWA MIEZI MITATU KUZUIA SHAMBULIZI LA DUBE DHIDI YA SIMBA

 Na Ally Mandai.

Mwamuzi msaidizi namba mbili (2) wa mchezo tajwa hapo juu, Hamdan Said kutoka Mtwara amefungiwa miezi mitatu (3) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu ambapo katika dakika ya 61 ya mchezo aliashiria kuwa mchezaji Prince Dube wa klabu ya Young Africans alikuwa katika eneo la kuotea, hivyo kusimamisha shambulizi ambalo klabu ya Young Africans ilikuwa inafanya langoni mwa Simba.

Hata hivyo, taarifa ya wataalam wa kutafsiri sheria za mpira wa miguu, baada ya kufanyia tathmini video ya tukio hilo, imebainisha kwamba mchezaji huyo hakuwa katika eneo la kuotea wakati mpira huo unapigwa kuelekea kwake.

Adhabu hii ni kwa mujibu wa Kanuni ya 42:1(1.8) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti kwa Waamuzi.

TANGAZA NASI SASA,UWAFIKIE MAMILIONI YA WATEJA:Piga 0654414804. 



Post a Comment

0 Comments