MVUA KUBWA YAZUIA MECHI YA TRA VS SIMBA SC

 Na Ally Mandai.

Mechi ya Ligi Kuu ya NBC kati ya wenyeji TRA United na Simba SC imeahirishwa baada ya uwanja wa 'Sheikh Amri Abeid Stadium' kujaa maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha eneo hilo. Hali ya uwanja huo ilifanya iwe vigumu kwa mechi hiyo kuchezwa kama ilivyopangwa katika ratiba ya NBC Premier League.

Maafisa wa mechi pamoja na kamati ya waamuzi walilazimika kukagua uwanja huo kabla ya kufanya uamuzi wa kuahirisha pambano hilo, wakibaini kuwa maji yaliyotuama yangeweza kuhatarisha usalama wa wachezaji pamoja na kuathiri ubora wa mchezo. 

Mashabiki waliokuwa tayari kushuhudia pambano hilo kali walibaki wakisubiri maamuzi rasmi kuhusu lini mechi hiyo itachezwa tena.

Uongozi wa ligi unatarajiwa kutangaza tarehe mpya ya kuchezwa kwa mchezo huo mara baada ya tathmini ya hali ya uwanja kukamilika. 

Pambano hilo lilitarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na kiwango kizuri cha timu zote mbili, hususan Simba SCambao wanaendelea kupambana kujiimarisha kwenye msimamo wa Ligi kuu.

TANGAZA NASI SASA,UWAFIKIE MAMILIONI YA WATEJA:Piga 0654414804. 



Post a Comment

0 Comments