TUME YA KUCHUNGUZA MATUKIO YA UVUNJIFU WA AMANI YAKUTANA NA JAJI WARIOBA


  TUME ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, leo Januari 14, 2026, imekutana na Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu, Joseph Warioba.
-
Mkutano huo wa Tume na Mzee Warioba, ambaye pia ni Jaji mstaafu ulifanyika katika ofisi za Tume hiyo zilizopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini, Dar es Salaam.
-
Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo.


 

Post a Comment

0 Comments