Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Gairo leo ikiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Mhe. Danistan Mwendi, kwa imepokea na kujadili masuala mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na kutathmini utekelezaji wa Ilani ya CCM wilayani humo kupitia taasisi zote za Serikali zinazotolewa huduma kwa wananchi.
Katika kikao hicho, wajumbe wamepokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM iliyowasilishwa na Mhe. Japhari kubecha Mkuu wa Wilaya ya Gairo v ambapo wamepongeza hatua zilizofikiwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo hususan katika sekta za elimu, afya, maji na miundombinu.
Halmashauri Kuu imeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi inayoendelea, ikiwemo ujenzi na ukamilishaji wa vituo vya afya, shule, miradi ya maji pamoja na maboresho ya miundombinu ya barabara, na kuwataka watendaji kuendelea kusimamia miradi hiyo kwa kuzingatia thamani ya fedha na ubora wa kazi.
Aidha, kikao hicho kimewasisitiza viongozi na watendaji kuendelea kushirikian, sambamba na kuimarisha mshikamano kwa maslahi ya wananchi wa Wilaya ya Gairo.
Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Gairo imesisitiza umuhimu wa kuendeleza nidhamu, uwajibikaji na usimamizi madhubuti wa rasilimali za umma ili kuhakikisha maendeleo endelevu yanawafikia wananchi wote.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

0 Comments