FAR RABAT WAMESHINDWA MFUPA WA YANGA,AL AHLY WATAWEZA NEW AMAAN COMPLEX

 Yanga imepoteza mechi ya mzunguko wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa mabao 2-0 na wenyeji wao Al Ahly katika mchezo uliopigwa nchini Misri.

Mabao ya Al Ahly yalifungwa na Mahmoud Trezeguet, aliyepachika bao la kwanza dakika ya 45+3 kabla ya kurejea tena dakika ya 75, na kuihakikishia timu yake ushindi muhimu.

Kwa mujibu wa ratiba, timu hizo zitakutana tena katika mechi ya mzunguko wa nne itakayochezwa mwishoni mwa wiki ijayo kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar.

Matokeo hayo yanaifanya Al Ahly kuendelea kuongoza msimamo wa Kundi B kwa kufikisha pointi 7, huku Yanga ikishika nafasi ya pili ikiwa na pointi 4. Timu za FAR Rabat na JS Kabylie zinabaki na pointi 1 kila moja.

Mechi ya marudiano Zanzibar inatarajiwa kuwa ya ushindani mkubwa, huku Yanga ikihitaji matokeo chanya ili kujiweka vizuri katika mbio za kufuzu hatua inayofuata.




 

Post a Comment

0 Comments