MBETO AMVAA OMO AKIMTAKA AACHE MAKEKE YAKE

  Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 

Chama Cha  Mapinduzi  kimesema kwa mujibu wa Sheria  hakuna chama  chochote  cha Siasa ,Vyombo vya habari au Taasisi  yoyote  yenye Mamlaka ya kutangaza matokeo ya Uchaguzi bila  idhini ya  Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Pia chama hicho kimesisitiza kuwa  Uchaguzi  katika nchi  yoyote duniani  ,  huongozwa kwa kanuni na  taratibu  za kisheria  si  kwa mtindo holela .

Msimamo huo   umetolewa na Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC Zanzibar,  Idara  ya Itikadi ,Uenezi na Mafunzo,  Khamisi  Mmbeto Khamis,  wakati  akijibu hoja zilizotolewa na mgombea urais wa ACT  Wazalendo ,Othman Masoud Othman  .

Othman mara baada ya kuchukua  fomu  ya kuwania Urais, amesikika akiikosoa Sheria ya Kura ya mapema akitishia na kutaka iisitumilke . 

Mbeto  akijibu hoja hiyo alisema ,sheria hiyo haikiutungwa aidha na Malaika ,majini au Mashetani , bali  imetungwa na binadamu  waliopewa dhamana ya  kutunga na kupitisha sheria.

Alisema sheria  hiyo itaendelea  kutumika Zanzibar  hadi pale  Baraza la Wawakilishi Zanzibar,   litakapofanya mabadiliko mengine kwa utaratibu  halali . 

"Hauna Sheria nzuri au mbaya ikiwa imeshatungwa pia  imepitishwa na  Baraza la  Wawakilishi Zanzibar. Sheria  ya Kura ya mapema imeridhiwa na chombo  hicho  .Haikutungwa katika ofisi  ya chama chochote  cha Siasa" Alisema Mbeto 

Aidha, Katibu  huyo Mwenezi alisema ni wazi  ACT kupitia  mgombea wake  wa urais , kimebaini kushindwa kwa kuona  maendeleo  yalivyoshamiri huku wananchi wakisifu uongoozi wa Rais Dk  Hussein Ali  Mwinyi .

"Hayupo  mwenye ubavu  wa kuzuia watu wasipige kura ikiwa sheria inataka hivyo . Atakaewatisha, kuwazuia au kutaka kuwapiga Wapiga Kura wasifike vituoni watadhibitiwa  na mkono wa sheria "Alisema Mbeto 

Pia katibu  huyo  Mwenezi  aliongeza kusema kuwa ikiwa  Othman ameshajua kuwa hawezi kushinda ,si kosa kwake  kutangaza kuwa amekubali kushindwa .

"Sheria  anayoipinga  imetungwa na Wajumbe halali wa Baraza la wawakilishi Zanzibar . Inawezaje kufutwa leo  ikiwa chombo hicho kimevunjwa kisheria ?" Alihoji  Mbeto 

Mwenezi  huyo alisema anachokitaka Othman  ni kuwashawishi  Vijana  wa ACT  ili walete ghasia na fujo kwa kisingizio  cha Sheria ya kura za mapema ambayo imekuwa ikitumika katika Mataifa mengi  duniani.


Post a Comment

Previous Post Next Post

Contact Form