Mwenyekiti wa
(CHADEMA), Tundu Lissu anatarajiwa kuendelea kumhoji shahidi wa 16 wa
Upande wa Jamhuri, ACP Amini Mahamba kesho Agosti 11, 2026 katika kesi
ya uhaini inayomkabili.

Kesi hiyo inaendelea katika Mahakama Kuu,
Masjala Ndogo Dar es salaam ambapo leo Agosti 10, Lissu ameanza kumhoji
shahidi huyo kwa maswali ya dodoso (cross-examination).
Katika
hatua hiyo, Lissu amesema ana maeneo 54 anayokusudia kumuuliza shahidi
huyo, akidai kuna utata kati ya ushahidi alioutoa Mahakamani na maelezo
yake ya awali.
Miongoni mwa maeneo aliyoyaibua ni elimu na uzoefu
wa shahidi huyo ndani ya Jeshi la Polisi, namna alivyopanda vyeo pamoja
na baadhi ya maelezo aliyowahi kuyaandika.
Katika mahojiano
hayo, Lissu pia aliomba maelezo ya shahidi huyo yapokelewe kama
kielelezo ambapo baada ya mvutano wa muda, Mahakama ilipokea maelezo
hayo kwa upande wa Lissu.
Lissu aliendelea kumuuliza shahidi
kuhusu baadhi ya taarifa ambazo amedai zilikuwepo katika ushahidi wake,
lakini hazikuonekana kwenye maelezo yake ya awali.
Kesi imeahirishwa hadi kesho saa tatu asubuhi, ambapo Lissu ataendelea na maswali ya dodoso kwa ACP Mahamba.
Lissu
anakabiliwa na shtaka moja la uhaini kinyume na Kifungu cha 39(2)(d)
cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, linalohusishwa na maneno aliyoyatamka
kuhusu kusudio la kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
0 Comments