Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameendelea kujitetea mbele ya Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam katika shauri linalohusu maombi yaliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), huku akiiomba mahakama kutoa uamuzi unaolinda haki zake za kikatiba.
BOFYA HAPA:UREJESHE HESHIMA CHUMBANI NA VIKSI LOTION
Akiwasilisha hoja zake mbele ya jopo la majaji watatu, Lissu alidai kuwa shauri lake limecheleweshwa kwa makusudi kwa siku 139 tangu Februari 24, 2026, jambo alilosema limemletea usumbufu mkubwa na kumfanya aendelee kubaki mahabusu bila sababu za msingi.
Kutokana na hali hiyo, Lissu aliiomba Mahakama ya Rufani iamuru DPP kumlipa fidia kwa usumbufu alioupata, akisisitiza kuwa ucheleweshaji huo unatokana na mbinu za kisheria zinazotumiwa na upande wa Jamhuri ambazo zimekuwa zikikwamisha mwenendo wa shauri hilo.
Aidha, Lissu alisema ametimiza mwaka mmoja na miezi mitatu tangu akamatwe kwa tuhuma za uhaini, na kuiomba Mahakama ya Rufani iyatupilie mbali maombi ya DPP kwa madai kuwa hayana maslahi ya umma, huku akiitaka mahakama itoe haki kwa kuamuru alipwe fidia kutokana na ucheleweshaji wa shauri hilo.



0 Comments