SERIKALI YASISITIZA USHIRIKIANO NA SEKTA BINAFSI KUKUZA AJIRA NA USAWA WA KIJINSIA

 Na. Mwandishi wetu - DSM

Serikali inaendelea kuthamini mchango wa sekta binafsi katika kukuza Uongozi bora, Ajira stahiki pamoja na kuimarisha usawa wa kijinsia mahali pa kazi.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Rahma Kisuo, wakati akifungua Kongamano la Women’s Leadership Forum Machi 28, 2026 jijini Dar es Salaam.

Mhe. Kisuo amesema mafanikio ya taifa yanategemea ushirikiano madhubuti kati ya Serikali na waajiri katika kujenga mazingira ya kazi yaliyo salama, jumuishi na yanayoheshimu haki za wafanyakazi wote bila ubaguzi.

Aidha, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuongoza juhudi za kuweka sera na mikakati inayowawezesha wanawake na vijana kushiriki kikamilifu katika uchumi wa taifa.



Post a Comment

0 Comments