Na Ally Mandai.
Bodi ya Wakurugenzi ya Simba imesikitishwa na vitendo vya baadhi ya watu kuitisha mkutano na kutoa maneno ya kashfa na kauli zisizo na staha kwa Mwekezaji wa Simba, Ndugu Mohammed G. Dewji.
Vitendo hivyo visivyo vya kiungwana, havikubaliki. Uongozi wa Klabu unatoa pole kwa Ndugu Mohammed Dewji.
Aidha, uongozi wa Klabu umeliandikia Jeshi la Polisi kuchukua hatua kali za kisheria kwa wote waliohusika katika mkutano huo ama kula njama na kuwafikisha katika vyombo vya dola kwa makosa ya jinai.
Bodi inasisitiza kuwa haitabariki wala kuvumilia mtu yoyote atakaeharibu taswira ya Klabu kwa namna yoyote ile.

.jpg)

0 Comments