Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Dkt. Abubakar Zubeir bin Ally, amesema mwanamke aliyefiwa na mumewe anaweza kuendelea kutekeleza majukumu muhimu yanayomhitaji binafsi akiwa katika kipindi cha eda, endapo hakuna mtu mwingine anayeweza kumwakilisha.
Mufti Zubeir ameeleza kuwa hatua hiyo inaruhusiwa kwa kuzingatia masharti na taratibu zilizowekwa na Sheria ya Kiislamu kuhusu kipindi cha eda.
Akitoa mfano wa Rais Samia Suluhu Hassan, Mufti Zubeir amesema kuwa licha ya Rais kuwa katika kipindi cha eda, anaweza kuendelea kutekeleza majukumu ya kitaifa ambayo yanamhitaji yeye mwenyewe, ikiwa hakuna mtu mwingine anayeweza kuyatekeleza kwa niaba yake.
Amesisitiza kuwa utekelezaji wa majukumu hayo unapaswa kufanyika kwa kuzingatia masharti na taratibu za eda kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu.

0 Comments