Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, imebaini uwepo wa taarifa za uongo zinazotengenezwa kwa sura ya taarifa rasmi na kusambazwa mitandaoni zikidaiwa kutoka Ikulu au kuhusishwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kurugenzi inaujulisha umma kuwa taarifa zote rasmi kuhusu shughuli za Mheshimiwa Rais hutolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, kulu, kupitia tovuti na kurasa rasmi zifuatazo:
.Instagram: Ikulu Tanzania: @Ikulu_mawasiliano;
· Facebook: Ikulu Tanzania: ikulu.mawasiliano; na
. Tovuti: http//tewry.fkulw.go.tz,
Hivyo, Kurugenzi inasisitiza umma kuthibitisha taarifa yoyote kumhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vyanzo hivyo kabla ya kuzipokea au kuzisambaza.
Aidha, Kurugenzi inaukumbusha umma kuwa utengenezaji na usambazaji wa taarifa za uongo kwa kutumia jina, nembo au utambulisho wa Rais au Ikulu ni kosa kwa mujibu wa Kifungu cha 15 na 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (Sura ya 443).
0 Comments