Waziri Mkuu
wa Israel Benjamin Netanyahu amesema hawakubaliani na mpango wa Gaza
uliotangazwa na Marekani na kuungwa mkono na kundi la Hamas na kupingana
kwa kiasi fulani na mshirika wake Rais Donald Trump.

Waziri Mkuu
Netanyahu ameutupilia mbali mpango huo, kuhusu Gaza uliotangazwa na
Rais Trump mwezi uliopita na kusisitiza kwamba Jeshi la Israel
halitaondoka wala kuondoa chochote kwenye eneo hilo la Kipalestina hadi
Hamas itakaponyang'anywa kikamilifu silaha.
Netanyahu aliliambia
Baraza la Mawaziri kwamba Israel imeukataa waraka huo wa vipengele 15
ingawa alisema bado wanajadiliana na Marekani mikakati kwa ajili ya
Gaza, matamshi ambayo pia aliyatoa wiki iliyopita.
“Kuhusiana na
masuala fulani yanayojitokeza kwenye taarifa za habari hivi karibuni,
nataka kusahihisha hapa: Israel inakataa hati ya vipengele 15. Nilisikia
watu wakisema: 'Haukusema.' Kwa hivyo nasema tena: Israel inakataa hati
ya vipengele 15 IDF haitaondoa chochote hadi Hamas itakaponyang'anywa
silaha. Na ninaposema kuwanyang'anya silaha Hamas, namaanisha silaha
nzito, silaha zisizo nzito.... silaha zote," alisema Netanyahu.
Netanyahu
pamoja na kuukataa mpango huo bado alimuelezea Trump kuwa ni "rafiki
mkubwa zaidi wa Israel katika Ikulu ya White House," ingawa aliweka wazi
kuwa alikuwa tayari kumpinga pale inapotakikana, na kuongeza kuwa
Israel tayari ilikuwa imewasilisha pingamizi kwa Marekani.
Alipouwasilisha,
alisema kwamba vikosi vya Israel vingeondoka baada ya zoezi la
kuwapokonya silaha Hamas kukamilika. Vikosi hivyo vinadhibiti zaidi ya
nusu ya eneo hilo dogo la Palestina lenye kama wakaazi milioni 2 na
ambalo kwa kiasi kikubwa limeharibiwa na mashambulizi ya Israel.
0 Comments