Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mnyaa Mbarawa amesema Serikali ya Tanzania inaendelea kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati ya miundombinu ya usafiri inayolenga kuimarisha huduma za usafirishaji katika Ushoroba wa Kati (Central Corridor), huku mafanikio makubwa yakionekana katika reli ya kisasa ya SGR, Bandari ya Dar es Salaam na usafiri wa majini.
Akizungumza katika Mkutano wa 15 wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Ushoroba wa Kati (ICM) unaofanyika Dar es Salaam leo Juni 18, 2026, Prof. Mbarawa amesema ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR katika sehemu mbalimbali za Dar es Salaam, Mwanza, Tabora, Kigoma pamoja na Uvinza hadi Musongati nchini Burundi utaongeza kwa kiasi kikubwa muunganiko wa kikanda, biashara na ushirikiano wa kiuchumi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Amesema tangu kuanza kwa huduma za usafiri wa abiria wa SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma mwezi Juni 2024, Shirika la Reli TANZANIA.

0 Comments