RAZALOUS MWAKIPOSA ‘ZIMWI’ AIBUKA KIDEDEA UCHAGUZI WA WENYEVITI DAR

 WAJUMBE kutoka wilaya tano za Mkoa wa Dar es Salaam, wamemchagua Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Dovya, Kata ya Bunju, ambaye pia ni Mwenyekiti wa wenyeviti wa  serikali za mitaa Wilaya Kinondoni, Razalous Mwakiposa maarufu kama Zimwi, kuwa Mwenyekiti wa  Wenyeviti wa mkoa huo.

Aidha wajumbe hao kutoka Wilaya za Ubungo, Kinondoni, Ilala, Kigamboni na Temeke,  wamemchangua Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa  Mwongozo , wilayani Ubungo,  Pipino Pipino  kuwa Katibu wa Wenyeviti wa mkoa huo.

Viongozi hao wamechaguliwa Katika uchaguzi uliofanyika  jijini Dar es Salaam, ambapo  kwa nafasi ya  mwenyekiti  ilijumuisha  wagombea watatu ambao niJuma  Abas, Consolata Rwiza na  Zimwi.

Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi  Kambi Sande, amesema jumla ya wajumbe  ni 37 na Zimwi amepata 
 kura 24, Abas kura   mbili huku  Rwiza akipata kura 11  ambapo jumla ya wapigakura wakuliwa 37.

"Kwa mamlaka niliyopewa ninamtangaza Razalous Mwakiposa kuwa Mwenyekiti wa Wenyeviti wa Mkoa wa Dar es Salaam,"amesema Sande.

 Akizungumza baada ya kuchaguliwa, Zimwi amewashukuru wajumbe kwa imani kubwa waliyompa na kwamba  ajenda yake kuu katika uongozi ni kusimamia  utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  na kutetea maslahi ya wenyeviti.

Kuhusu uchaguzi wa nafasi ya katibu, Pipino ameibuka mshindi kwa kuvuna kura  20, ambapo  Athuman Gereza amepata  kura 17 kati ya kura 37 zilizopigwa.


 

Post a Comment

0 Comments