Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba
amewasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri
Mkuu pamoja na Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha 2026/2027, yenye jumla
ya shilingi trilioni 12.5 (12,502,356,160,000)
Akiwasilisha hoja
hiyo leo Aprili 1, 2026, Bungeni Jijini Dodoma, Dkt. Nchemba alisema
kuwa kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 8.73 zimetengwa kwa matumizi
ya kawaida, huku shilingi trilioni 3.77 zikielekezwa katika utekelezaji
wa miradi ya maendeleo.
Dkt. Mwigulu amefafanua kuwa bajeti hiyo
inalenga kuimarisha utoaji wa huduma za Umma pamoja na kusukuma mbele
agenda ya maendeleo katika taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu
na Bunge.
Kwa upande wa mapato, Waziri Mkuu amelieleza Bunge kuwa
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa zinatarajia
kukusanya jumla ya Shilingi Trilioni 2.34 (2,336,528,152,302.47) ambapo
jumla ya makusanyo na maduhuli ya ofisi yake ni Shilingi Trilioni 2.4
(2,411,548,152,302.47) ambazo zinatarajiwa kukusanywa.
Aidha,
Dkt. Mwigulu amebainisha kuwa kiasi cha Shilingi Trilioni 12.268
(12,268,472,643,000) kitatumika mahsusi kugharamia shughuli za kawaida
na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Mikoa na Mamlaka za
Serikali za Mitaa, hatua inayotarajiwa kuimarisha utoaji wa huduma kwa
wananchi.
0 Comments