KAGOMA AONGEZA MIAKA 2 KUITUMIKIA SIMBA SC

 Na Ally Mandai.


Kiungo mkabaji wa Simba SC,Yusuph Kagoma, leo amesaini rasmi mkataba mpya wa kuendelea kubaki ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi. 

Makubaliano hayo mapya ni ya miaka miwili, yakionyesha imani kubwa ambayo klabu hiyo inaendelea kuwa nayo kwa nyota huyo wa safu ya kiungo. 

Kagoma amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Simba, hasa katika kuimarisha eneo la kiungo wa ulinzi na kusaidia timu kupata utulivu katikati ya uwanja. 

Kwa kusaini mkataba huo mpya, Kagoma ataendelea kuitumikia Simba hadi mwaka 2028 huku mashabiki wakitarajia mchango mkubwa zaidi katika misimu ijayo. 

TANGAZA NASI SASA,UWAFIKIE MAMILIONI YA WATEJA:Piga 0654414804. 





Post a Comment

0 Comments