Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amemtembelea na kumjulia hali aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Joseph Sinde Warioba, katika makazi yake yaliyopo Mbezi Juu, jijini Dar es Salaam.
Ziara hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya kuonesha heshima, kuthamini mchango wa viongozi wastaafu pamoja na kufuatilia hali ya afya na ustawi wao. Katika mazungumzo yao, viongozi hao walipata fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Taifa.
Mhe. Dkt. Nchimbi alimtakia afya njema na maisha marefu Mhe. Warioba, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuthamini busara, uzoefu na mchango wa viongozi waliolitumikia Taifa kwa uadilifu na uzalendo.
Kwa upande wake, Mhe. Warioba alimshukuru Makamu wa Rais kwa kumtembelea na kuonesha upendo pamoja na kujali hali yake, akieleza kuwa hatua hiyo ni ishara ya mshikamano na heshima kwa viongozi waliostaafu kulitumikia Taifa.


.jpeg)


0 Comments