Na Ally Mandai.
Klabu
ya KMC rasmi imetangaza kumfuta kazi aliyekua kocha wa klabu hiyo
Abdallah Mohamed "Bares" pamoja na benchi lake la ufundi.
Taarifa
iliyotolewa na KMC imeeleza kuwa “Klabu ya KMC imekaa na kukubaliana
pande zote na kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba na kocha Abdallah
Mohamed "Bares" pamoja na benchi lake la ufundi”
Aidha taaifa
hiyo imeongeza kuwa Tunatambua na kuthamini jitihada walizofanya katika
kuboresha utendaji wa timu, ndani na nje ya uwanja, kwa ngazi ya
mchezaji
mmoja mmoja na timu kwa ujumla.
KMC leo imepoteza
mchezo wake dhidi ya Mbeya City kwa mabao 3-2 na wanaburuza mkia kwenye
msimamo wa ligi Kuu ya NBC wakiwa na jumla ya alama 8.
0 Comments