JMAT YASIFIA MARIDHIANO YA TAIFA

 Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Dkt. Maasa Ole Gabriel, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa busara na hekima zake zilizoifanya Tanzania kuendelea kuwa salama na yenye amani

Ameipongeza hatua ya kuanzisha mchakato wa maridhiano kupitia Tume ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Askofu Dkt. Maasa ametoa kauli hiyo Aprili 3, 2026 katika ofisi za Jumuiya hiyo jijini Arusha, wakati taifa likisubiri kupokea ripoti ya tume hiyo. Amesisitiza kuwa ni umuhimu kwa Watanzania kuendelea kuwa watulivu na kudumisha mshikamano uliopo nchini.

Amesema ripoti hiyo itajumuisha maoni ya makundi mbalimbali yaliyoguswa na matukio hayo, wakiwemo vijana, viongozi wa dini na siasa pamoja na wanajamii wengine. Ameongeza kuwa JMAT itaendelea kusisitiza umuhimu wa kulinda tunu za taifa, ikiwemo amani, upendo na mshikamano.

Aidha, amewahimiza wananchi kusubiri kwa utulivu hatua zitakazochukuliwa baada ya Rais kupokea na kupitia mapendekezo yaliyomo kwenye ripoti hiyo, akieleza kuwa umoja na amani ni rasilimali muhimu kwa maendeleo ya taifa.


 

Post a Comment

0 Comments