Tibirinzi, Kusini Pemba | 11 Machi 2026
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amejumuika na waumini wa dini ya Kiislamu pamoja na wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba katika futari ya pamoja aliyowaandalia, iliyofanyika katika Uwanja wa Kufurahishia Watoto Tibirinzi.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi.
Akizungumza na wananchi, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa utaratibu wa kufutari pamoja unaimarisha upendo, mshikamano na umoja miongoni mwa jamii, na kuwashukuru wote walioshiriki katika futari hiyo.
Futari hiyo imewakutanisha wananchi kutoka makundi mbalimbali wakiwemo mayatima, wajane, watu wenye ulemavu, walimu wa madrasa, masheikh na maimamu wa Mkoa wa Kusini Pemba.
Kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Kusini Pemba, Shehe Hassan Shaaban amemshukuru Rais Dkt. Mwinyi kwa matendo mema, fadhila na wema anaowaonesha wananchi, ikiwemo kuwaandalia futari hiyo, na kumtakia uongozi mwema na mafanikio.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Wete, Ndugu Abdalla Ali Rashid, akizungumza kwa niaba ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, amempongeza Rais Dkt. Mwinyi kwa juhudi zake za kudumisha amani nchini pamoja na hatua ya Serikali kuweka bei elekezi kwa bidhaa za chakula, akieleza kuwa wafanyabiashara wametekeleza agizo hilo kikamilifu.

.jpeg)

0 Comments