MHE. MWINJUMA AFIKISHA POLE YA RAIS SAMIA KWA MWANAMUZIKI BICHUKA

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Mhe. Hamis Mwinjuma amemtembelea na kumjulia hali Mwanamuziki nguli  Mzee Hassan Rehani Bichuka nyumbani kwake Sinza Mori, jijini Dar es Salaam.

Mhe Mwinjuma alimtembelea mwanamuziki huyo Machi 9, 2026 na kufikisha salamu kutoka kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  ambapo alisema Rais Samia anamtakia Bichuka kila la heri na anamuombea afya njema ili apone haraka.

Naibu Waziri Mwinjuma  alimkabidhi Mzee Bichuka  Shilingi Milioni 10  taslimu, ikiwa ni mkono wa pole uliotolewa na Rais Samia kwa ajili ya kumtia moyo katika kipindi hiki cha matibabu.


Post a Comment

0 Comments