TANI 23,000 ZA MBOLEA YA UREA KUSAMBAZWA KWA WAKULIMA NCHINI

 Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) imesaini Mkataba na Kampuni ya Sea Energy Group Company ya Dubai tarehe 25 Juni 2025, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mauziano ya mbolea aina ya UREA tani 23,000.

Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Bw. Samuel Mshote amesema kuwa lengo la TFC kwa mwaka wa fedha 2024/25 ilikuwa kusambaza mbolea ya ruzuku tani 100,000 na hadi sasa TFC imesambaza tani 31,500 ya mbolea ya kupandia ya DAP, tani 35,000 za mbolea ya kukuzia ya UREA N46% na tani 59,127 za mbolea kwaajili ya zao la tumbaku.

Pia katika kupunguza gharama za uagizaji wa mbolea TFC imeanza kujishughulisha na uwekezaji wa viwanda, kwa kuagiza mitambo na kuifunga kwa ajili ya kuchanganya mbolea kulingana na aina ya udongo.

Mbolea ya UREA N46% ni maalum kwa ajili ya kukuzia mazao itauzwa kwa wakulima kwa bei ya ruzuku kwa utaratibu wa ruzuku ya Serikali. Na itasambazwa kwa wakulima wote nchini.

Kwa upande wake, Bw. Dean Tavakoli, Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Sea Energy Group Company ameishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Kilimo na kuahidi kuleta mbolea yenye viwango na gharama nafuu kwa mkulima.






 

Post a Comment

0 Comments