Spika wa Bunge na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson ameweka Jiwe la Msingi la ujenzi ya Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Bunge.
Tukio hilo limefanyika leo tarehe 26 Juni, 2025 eneo la Kikombo ambapo ndipo shule hiyo inajengwa na limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waheshimiwa Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge.
Mheshimiwa Spika amesema shule hiyo itagharimu zaidi ya shilingi bilioni 3 na amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuchangia ili kukamilisha mradi huo.
Mheshimiwa Spika amesema fedha za kuanza mradi huo zimetokana na michango mbalimbali kutoka kwa wadau na Waheshimiwa Wabunge na baadhi zilikusanywa katika Marathoni ya Bunge na Mabonanza mbalimbali.
Amesema Bunge la Tanzania likiwa ni wawakilishi wa makundi yote wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha mtoto wakike na wakiume wanapata fursa sawa kwa kuwapatia elimu endelevu.
Bunge la Kumi na Moja lilishajenga Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Bunge ya mchepuo wa sayansi kwa lengo la kuendelea kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu nzuri na bora.

.jpeg)

.jpeg)


.jpeg)

0 Comments