Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema
Serikali imefanya uwekezaji mkubwa wa vifaa tiba na wataalaam wenye
utaalam wa juu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ili iweze kutoa
huduma bora zinazokidhi viwango vya kimataifa

Rais Dkt. Samia
ameyasema hayo leo wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali walioteuliwa
hivi karibuni kushika nafasi mbalimbali katika viwanja vya Ikulu,
Chamwino mkoani Dodoma.
Rais Dkt. Samia amemtaka Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali hiyo kuendelea kusimamia utoaji wa huduma katika
hospitali hiyo kubwa na kongwe, kiongozi katika matibabu ya ubingwa
bobezi na utalii tiba katika Kanda wa Afrika Mashariki na Kati.
“Muhimbili
inahitaji professionalism na administative skills, nenda kaendeleze
pale alipoishia Prof. Janabi, nimepitia wasifu wa watu wengi lakini
nikaona wewe Dkt. Delilah Kimambo ndio unafaa kuiongoza hospitali hiyo,
nakutakia kila la heri katika kutekeleza majukumu yako” ameongeza Rais
Dkt. Samia.
Aidha, Rais Dkt. Samia amebainisha kuwa serikali
imepata fedha kwa ajili ya maboresho ya hospitali hiyo husani katika
eneo la ujenzi wa miundombinu ya majengo ikiwa ni muendelezo wa mikakati
ya kuboresha sekta ya afya hapa nchini.
Dkt. Delilah Kimambo
aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia
Suluhu Hassan kuwa Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Juni 16,
2025.
0 Comments