Naibu Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Mhe. Deus Sangu,
ametembelea banda la PSSSF katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
kitaifa, yanayoendelea katika viwanja vya Chinangali jijini Dodoma na
kuupongeza Mfuko kwa utoaji huduma bora kwa wanachama.
“Ushiriki
wenu umeonyesha dhamira yenu ya kuwahudumia watanzania naamini mmeweza
kutoa elimu na hii ni moja ya mkakati wa kufikisha elimu kwa umma,
hongereni sana.” Alisema.
Alisema kwa sasa Mfuko umekuwa ukifanya
vizuri katika utekelezaji wa jukumu lake la msingi la ulipaji wa Mafao
na hata Mfuko umeimarika kiukwasi.
“Niwapongeze kwa kuweza kuufanya Mfuko huu kuwa himilivu kwa maana ya kutekeleza vema jukumu la ulipaji wa mafao,” alisisitiza.
Aidha, ameomba Mfuko kuendelea kuimarisha ushirikiano baina yao na wz
aajiri.“Ili
tuweze kwenda vizuri tuwapatie elimu wafanyakazi wanaokaribia kustaafu;
Najua hili mnalifanya, lakini likifanyika miezi sita kabla itasaidia
sana kuwawezesha watakapostaafu waweze kusimamia vema Mafao na zile
pensheni za kila mwezi ili waweze kumudu maisha baada ya utumishi.”
Alisema.
0 Comments