Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamsaka mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Mgore anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 na mkazi wa Ibanda, Kata ya Kirumba Wilaya ya Ilemela kwa tuhuma za mauaji ya mume wake aitwaye Amosi Faustine Paulo, miaka 31, dereva wa pikipiki na mkazi wa Ibanda aliyeuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani upande wa kisogoni.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi leo Juni 27, 2025
tukio hilo limetokea Juni 25,2025 majira ya saa 4.30 usiku huko katika
hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-Toure muda mchache wakati Amosi
Faustine Paulo alipofikishwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu ili kuokoa
maisha yake baada ya kujeruhiwa na kitu chenye ncha kali na mke wake
wakiwa chumbani kwenye nyumba ya Joseph Bukoma Misungwi iliyopo eneo la
Ibanda, Wilaya ya Ilemela walipokuwa wamepanga.

0 Comments