MAKONDA AFUNGUKA KUWA MKEKA WA JANA NI MPANGO YA MUNGU

 Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini mara mbili katika utumishi wake wa umma, akimteua kuwa Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na baadaye Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Akizungumza leo Juni 24, 2025, kwenye Jukwaa la Wanawake lililofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano (AICC) jijini Arusha, Makonda amesema hakuwa akitarajia kuwa hiyo ingekuwa hotuba yake ya kuaga ndani ya mkoa huo.

“Balozi (Dk Emmanuel Nchimbi), naomba kwa unyenyekevu mkubwa unifikishie salamu kwa Rais Samia kwa kuniamini mara mbili ndani ya utumishi wake wa urais tangu mwaka 2021, kuniteua kuwa msemaji wa Chama Cha Mapinduzi na Mkuu wa Mkoa wa Arusha…Sikutarajia leo itakuwa hotuba yangu ya kuaga,” amesema Makonda.

Mgeni rasmi katika jukwaa hilo alikuwa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi.

Post a Comment

0 Comments