Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ametumia fursa ya
hotuba ya kuhitimisha mkutano wa 19 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na kupongeza juhudi na mafanikio makubwa yaliyofanikishwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan,
katika kuimarisha uhusiano wa kimataifa na diplomasia ya uchumi.
Waziri
Mkuu Majaliwa amesema, maono ya Rais Samia katika kuifungua Tanzania
kiuchumi na kisiasa yameleta mafanikio makubwa kwa taifa, na kuiweka
nchi katika nafasi ya heshima na ushawishi katika majukwaa ya kimataifa.Katika
hotuba hiyo, Waziri Mkuu ametaja mafanikio kadhaa yaliyopatikana chini
ya uongozi wa Dkt. Samia, ikiwa ni pamoja na ushiriki wa Tanzania katika
mikutano ya kimataifa yenye umuhimu wa kiuchumi na kisiasa kama vile
Mkutano wa Wakuu wa Nchi Tajiri Duniani (G20) uliofanyika Rio de
Janeiro, Brazil na Mkutano wa COP 29 kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi.
Ushiriki huu umeimarisha ushirikiano wa kimataifa na nafasi ya Tanzania
duniani.
Aidha, Tanzania imeandaa mikutano mikubwa ya kimataifa
ikiwemo Africa Energy Summit 2025 na Africa Food Systems Summit 2023,
ambayo imetoa fursa kwa nchi kujitangaza kiuwekezaji, kubadilishana
maarifa na kufungua milango ya ushirikiano mpya wa kimkakati.
Kupitia
ziara za kimataifa na mapokezi ya viongozi wakuu kutoka nje ya nchi,
Tanzania imeweza kusaini mikataba muhimu ya maendeleo. Miongoni mwa
mafanikio hayo ni makubaliano kati ya Tanzania, Zambia na China ya
kufufua reli ya kihistoria ya TAZARA, hatua inayotarajiwa kuboresha kwa
kiwango kikubwa huduma za reli na uchumi wa ukanda huu.
Vilevile
Waziri Mkuu amelieleza Bunge kuwa, Rais Samia pia amepokea rasmi
Uenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC. Chini ya uongozi
wake, Tanzania imesimamia kwa mafanikio uangalizi wa chaguzi katika
nchi mbalimbali za Kusini mwa Afrika kama Botswana, Mauritius, Msumbiji
na Namibia.
0 Comments