MAANDAMANO KENYA YAPELEKEA VIFO VYA WATU 16

 Watu 16 wamefariki dunia Nchini Kenya hadi kufikia jana Jumatano wengi wao wakidaiwa kuuawa kwa risasi na polisi, wakati wa maandamano makubwa yaliyoandaliwa kuadhimisha mwaka mmoja tangu maandamano ya kupinga Mswada wa Fedha wa 2024 uliosababisha uvamizi wa Bunge la Taifa.

Katika maandamano hayo yaliyofanyika kote nchini Kenya ikiwemo Nairobi, Mombasa, Kitengela, Kisii, Nyeri na Matuu, polisi walitumia mabomu ya machozi, maji ya kuwasha, risasi za mpira na silaha za moto kuwatawanya waandamanaji.



Post a Comment

0 Comments