SERIKALI kupitia Wizara ya Afya inaendelea kuimarisha huduma za afya za kinga na
huduma za afya ngazi ya jamii nchini, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa
Mpango Jumuishi wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii.

Hayo
yamebainishwa Juni19, 2025 na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Dkt.
Otilia Gowelle, alipofanya ziara ya kikazi mkoani Pwani ili kufuatilia
na kujionea hali ya utoaji wa huduma za afya na maendeleo ya mafunzo kwa
Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii (CHWs) katika mkoa huo.
Akiwa
katika Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi Kibaha, kinachotoa mafunzo
kwa CHWs, Dkt. Gowelle amewatia moyo na kuwataka kuzingatia masomo
yao kwa bidii ili kutoa huduma bora na zenye kuzingatia maadili na
viwango vya taaluma.
“Nawasihi msome kwa juhudi na maarifa ili
mkitoka hapa muwe tayari kutoa huduma zenye ubora, kuisaidia jamii
kukabiliana na changamoto za kiafya na kuchangia katika kufikia lengo la
afya kwa wote,” amesisitiza Dkt. Gowelle.
Sambamba na kutembelea
chuo, Dkt. Gowelle alifika katika kata ya Misugusugu, Halmashauri ya
Mji Kibaha, ambapo alikutana na CHWs walioko kazini na kushuhudia jinsi
wanavyotekeleza majukumu yao chini ya usimamizi wa wataalam wa zahanati
ya Misugusugu.
Alifurahishwa na namna wanavyoshirikiana kutoa huduma za kinga, tiba ya msingi, lishe na ustawi wa jamii.
Vilevile,
CHWs walipata nafasi ya kueleza mafanikio na changamoto wanazokumbana
nazo wakati wa utekelezaji wa majukumu yao, ikiwa ni pamoja na mahitaji
ya vitendea kazi na masuala ya usafiri ndipo Dkt. Gowelle akaahidi kuwa
Wizara itashirikiana na mamlaka za Serikali za Mitaa na wadau wa
maendeleo ili kuhakikisha changamoto hizo zinapatiwa suluhu na mazingira
ya kazi yanaboreshwa.
Katika ziara hiyo Dkt. Gowelle iliambatana na Mratibu wa Huduma za Afya Ngazi ya Jamii, Dkt. Norman Jonas Kyala.
Ziara
hiyo ni muendelezo wa juhudi za Serikali za kuimarisha huduma za afya
ngazi ya jamii kwa kuhakikisha utoaji wa huduma bora unaenda sambamba na
mafunzo na usimamizi endelevu katika ngazi zote za utekelezaji.
Serikali
kupitia Wizara ya Afya inaendelea kuimarisha huduma za afya za kinga na

0 Comments